Wasanii wanaotaka kutengeneza video kwenye vivutio vya utalii wanione - Dkt. Kigwangalla



Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangalla amesema wasanii watakaotaka kutengeneza filamu au video ya nyimbo zao kwenye vivutio vya utalii wamuone yeye, na atawapa vibali.

Waziri Kigwangala ameyasema hayo alipohudhuria hafla ya uzinduzi wa channel mpya ya utalii ya Shirika la Utangazaji ‹(TBC) iitwayo Tanzania Safari Channel, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Ameeleza kwamba jambo hilo litasaidia sana katika kutangaza vivutio vya utalii nchini na hivyo kuongeza idadi ya watalii wanaowasili nchini kila mwaka na kuongeza pato la taifa.

Sekta ya utalii inachangia asilimia 17.6 ya pato la taifa, lakini hatahivyo tunaona kuwa kiasi hiki hakitoshi.

Inaelezwa kuwa Tanzania kwa mwaka inapokea watalii takriban milioni 1.3, idadi ambayo serikali inalenga kuiongeza hadi kufikia milioni 2 ifikapo mwaka 2020.