Watu 43 wakamatwa Zanzibar, RC Ayoub atoa msimamo mkali

Jumla Ya watu  43 wnaosadikiwa kuwa omba omba wamekamatwa katika Mkoa wa Mjini Magharibi kati hao 13 wanatoka Tanzania Bara na wengine wanatoka katika Wilaya ya Magharibi “A”: na “B” Kisiwani Unguja.

Zoezi hilo limefanyika kufuatia kuenea kwa omba omba  wengi katika viunga vya Mkoa wa Mjini Magharibi na baadhi yao kuonekana kukaidi kuachana na biashra hio ya omba omba kufuatia maagizo mbali mbali ya yaliyotolewa hapo awali na uongozi wa Mkoa huo .

Akizungumza na watu hao katika ukumbi wa sebleni kwa wazee  Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema zoezi la kuwakusanya omba omba katika Mkoa wake limefanikiwa na kusisitiza shughuli hiyo ya omba omba haikubaliki katika maeneo hayo na endapo mtu yeyote antakaehusiaka anafanya shughuli hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA, PIA SUBSCRIBE