https://monetag.com/?ref_id=TTIb Waziri Mkuu aagiza barabara kupendezeshwa ili kuvutia watalii | Muungwana BLOG

Waziri Mkuu aagiza barabara kupendezeshwa ili kuvutia watalii


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kurekebisha na kupendezesha Barabara ya kutoka Uwanja wa Ndege wa JNIA hadi Kamata ili ivutie watalii, Dar es Salaam.

Waziri Majaliwa amezungumza hayo leo, alipohudhuria hafla na kuzindua chanel mpya ya utalii ya Shirika la Utangazaji (TBC) ijulikanayo kama Tanzania Safari Channel.

Ameeleza kwanza matengenezo ya barabara hiyo yalikuwa yamekwishaanza, lakini yaliishia njiani, hivyo kuagiza kuwa yaendelee na barabara hiyo iwe ya kuvutia. Majaliwa ameagiza vigingi vya bustani kando na katikati ya barabara hiyo virudishwe na taa za pembeni ya barabara hiyo ziwekwe na ziwake nyakati za usiku huku yakiwekwa matangazo ya kutangaza vivutio vipatikanavyo nchini.

Kuboreshwa kwa bustani hii pamoja na taa, kutapendezesha eneo hilo hususani kwa watalii wanaofika JNIA nyakati za usiku, wasikute jiji lina giza," aliongeza.

Waziri Mkuu ameeleza pia kuwa chaneli hiyo mpya ya utalii ya TBC itasaidia kutangaza vivutio vya utalii nchini na kuongeza idadi ya watalii wanaowasili nchini hadi kufikia lengo la serikali la kupokea watalii milioni 2 ifikapo mwaka 2020.