https://monetag.com/?ref_id=TTIb ZFA yafunguka kuhusu taarifa ya kuugua kwa wachezaji ghafla | Muungwana BLOG

ZFA yafunguka kuhusu taarifa ya kuugua kwa wachezaji ghafla



Na. Thabit Madai, Zanzibar.

Baada ya ZFA kupokea taarifa za kushtukiza na za kusikitisha za ugonjwa wa halfa wa kuharisha na kutapika mfululizo wa wachezaji wa timu mbili tofauti timu ya Mbuyuni na timu ya Mwenge uliozuka kwenye kambi zao walizofikia Mbuyuni wamefikia kambi ya kiwajuni Sc na Mwenge wamefikia kambi ya KMKM.

Hali hiyo imetokea jana usiku majira ya saa saba, baada ya viongozi wa ZFA kuwatembelea leo asubuhi katika kambi zote hali tuliyoikuta sio nzuri wapo walioruhusiwa kutoka hospitali na ambao bado wapo na wengine wanatibiwa hapo hapo kambini walipofikia.

Kwa hali na mazingira hayo ZFA imefikia uwamuzi wa kuzihairisha mechi mbili KMKM v Mbuyuni na mechi ya Malindi v Mwenge.

Mechi hizo zimeondolewa baada ya wachezaji zaidi ya kumi kwa kila timu kuwa kwenye hali mbaya ZFA inaomba samahani kwa usumbufu utakao jitokeza.

ZFA inawaombea kwa Allah wagonjwa wote wapone haraka waendelee na michezo yao na inawaomba wadau wote wa mpira wa miguu tuungane kipindi hichi kigumu kuwaombea wenzetu wapone haraka na atakae pata muda anaruhusiwa kuwatembelea kwenda kuwapa pole.

Imetolewa na:
ALAWI HAIDAR FOUM
KATIBU KAMATI YA MASHINDANO ZFA TAIFA.