.

1/12/2019

Beka Flavour akiri kuwa na ushamba wa mtotoMsanii wa Muziki, Bongo amekiri ushamba wa kuwa na mtoto baada ya mpenzi wake kujifungua mtoto.

Beka amesema kuwa mtoto wake huyo hajakuja kwa bahati mbaya amemfurahia na anampenda mwanae.

"Ujue mimi ni mtu ambaye watu wananishauri sana, alafu mimi nilikuwa na ushamba kidogo wa mtoto kwasababu umri wangu kidogo sio haba alafu 200,300 napata.Kwahiyo mtoto hajakuja kwa bahati mbaya nimemfurahia na nampenda sana mwanangu," alisema Beka.

Beka na Mpenzi wake, Happy mtoto wao mpaka sasa anakaribia kutimiza miaka mitatu tangu azaliwe.