BREAKING: Mgombea wa Upinzani atangazwa kuwa mshindi wa kiti cha Urais Congo


Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imemtangaza Mgombea wa Chama kikuu cha Upinzani Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa nafasi ya Urais kwa asilimia 38.57 ya kura zote.

Martin Fayulu ameshika nafasi ya pili huku Emmanuel Ramazani Shadary wa Chama tawala akiwa ameshika nafasi ya tatu. Hii ni mara ya kwanza Upinzani kushinda nchini Congo tangu nchi hiyo ilipopata Uhuru wake.

Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Ceni) Corneille Nangaa, alisema mapema Alhamisi kwamba Bw Tshisekedi alipata asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa na "anatangazwa mshindi wa urais mteule."

Tshisekedi alipata zaidi ya kura 7 milioni naye bw Fayulu akapata kura takriban 6.4 milioni, huku mgombea wa serikali Emmanuel Ramazani Shadary akipata takriban kura 4.4 milioni.

Rais Joseph Kabila anatarajiwa kuondoka madarakani baada ya kuongoza kwa miaka 18. Mgombea wake aliyemteua kuwakilisha muungano tawala Emmanuel Ramazani Shadary amemaliza wa tatu.