'Diamond alikuwa hajui kuimba vizuri'


Aliyekuwa Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Papaa Misifa amefunguka na kueleza kuwa muimbaji huyo alipomfuta kwa mara ya kwanza ili amsimamie kimuziki alikuwa hajui kuimba.

Akizungumza na Wasafi TV amesema kuwa kutokana na hilo alilazimika kumuweka pembeni Diamond kwa kipindi cha miaka miwili.

"Kwanza Diamond alipokuja kuomba kwangu alikuwa hajui kuimba vizuri, nilimuweka benchi miaka miwili kwa kumuangalia," amesema Papaa Misifa.

Utakumbuka Papaa ndiye aliyemtoa Diamond kimuziki na pia alionekana kwenye video ya kwanza ya muimbaji huyo inayokwenda kwa jina la Kamwambie.