.

1/08/2019

Fahamu madhara yatokanayo na kuangalia televisheni (TV) pekee


Kwa miaka ya hivi karibuni televisheni kimekuwa ni kitu cha kawaida ukilinganisha na miaka ya hapo nyuma, zamani itakumbukwa tulikuwa tunajaa sehemu moja tukiangalie television, sasa hivi kila mahali zimejaa television.

Ikumbukwe kuwa kazi ya telesheni ni kutupa habari na burudani zinazoendelea ulimwengu pote. Pamoja na kuwako na faida za kutazama television lakini yapo pia madhara yatokanayo na kuangalia television kwa muda mrefu  na madhara hayo  ni pamoja:

Hupoteza muda
Unapokaa na kuangalia televisheni ni wazi kuwa unatumia muda mwingi na wa muhimu sana ambao ungeutumia kufanya mambo ya msingi. Hii ni kutokana na sababu kuwa watu wengi hutazama televisheni kwa muda mrefu au hata siku nzima.

Utazamaji wa televisheni wa muda mrefu unaweza kukupotezea muda mwingi ambao ungeweza kuutumia kufanya kazi nyingine hasa zile zinazokuongezea kipato na maarifa.

Huathiri afya.
Binadamu hatakiwi akae kwa muda mrefu sana huku akitazama televisheni, hivyo kwa wale wanaokaa kwenye televisheni muda mrefu sana au hata siku nzima, hawazitendei haki afya zao.

Ni muhimu kufanya kazi za kuuchangamsha mwili au kufanya mazoezi mara kwa mara ili kulinda afya yako kuliko kukaa tu mbele ya televisheni.

Ikumbukwe pia tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa televisheni ni chanzo kikubwa cha ongezeko la unene kwa watu wengi duniani.

Kumbuka: sina maana ya kwamba usingalie television kabisa, hapana  bali unatakiwa kutenga muda malaamu wa kutazama televishion kuliko kukaa muda mwingi kutazama television.

Endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.