.

1/13/2019

Ishara zitazokuonyesha kama mwanaume uliyenaye anakupenda kweli


Siku zote ni lazima uelewe ya kwamba mwanaume kukwambia anakupenda tu hii haitoshi, bali yapo mambo ya msingi ambayo unatakiwa kuyoana kutoka kwa mwanaume huyo kama kweli anakupenda au anakudanganya tu.

Pia mara zote tunaambiwa wa watalamu wa masuala ya mahusiano kuwa upendo wa kweli huwa haujifichi bali huonekana kwa maneno na matendo pia.

Hivyo zifuatazo ndizo ishara zitakazokuonesha kama mwanaume uliyenaye anakupenda au aunakudanganya:

1. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni yule mwenye kukuonesha hisia zake za wazi za kimahusiano pasipo hata kukuonea aibu mpenziwe, hii ni kwa sababu kama nilivyosema hapo awali upendo wa kweli huwa haujifichi, hivyo kama kweli anakupenda kwa dhati zipo ishara za kihisia ambazo ni lazima uzione kutoka kwa mwanaume huyo.

Hisia za wazi ni kama vile matendo dhidi ya maneno ni lazima yaonekane waziwazi, hisia za wazi ni lazima mpenzi wako awe wazi kuwaeleza watu wengine kuhusu mahusiano yenu lakini pia hisia za wazi ni lazima mwanaume awe tayari kuongozana na wewe kila mahali pasipo kuona aibu yeyoto ile.

2. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni yule mwenye kukujali wewe kila wakati, hapa namaanisha ni lazima awe tayari kukusaidia katika shida na raha zote kila inapowezekana kuweza kukusaidia kufanya hivyo. Mapenzi ni hisia hivyo kila wakati ni lazima nafsi yako ione kuwa upo sehemu salama na haujutii kuwa mahala hapo.

3. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati na wewe ni yule mwenye kujali na kukukupa heshima zote unazostaili kuzipata kama mwanamke, hivyo kila wakati ni lazima atambue uwepo wako na kukupa uhuru pia wa kufanya mambo yako ya msingi na yakuleteayo mafanikio binafsi.

4. Mwanaume mwenye kutambua thamani ya mahusiano ni lazima atakuwa ni msikilizaji mzuri wa yale unayomwambia, hii ni kwa sababu wanaume wamejawa na misingi ya kibabe yaani yeye  anaamini yeye ndiyo kila kitu kitu hivyo haitaji ushauri wowote kutoka kwa mpenziwe. Mahusiano ya kweli hujengwa na pande zote mbili kuwa na mazungumzo na masikilizano yaliyo mwanana.

5. Mwanaume ambaye unamhitaji katika maisha yako ni yule ambaye hawezi kukuzuia kufanya kitu ambacho unakipenda kutoka moyoni mwako. Wanaweke wengi  wanakufa na uwezo mkubwa ulipo ndani yao hii ni kwa sababu ya wanaume walionao. Wengi huwazuia kufanya vile vitu wanavyofanya huku wakiamini ndio upendo wenyewe kitu ambacho si kweli hata chembe.

Hizo ni ishara za wazi ambazo zitakuonesha kama mwanaume uliyenaye anamapenzi ya kweli au anakupotezea muda tu. Endelea kutembelea Muungwana Blog.

Na. Benson Chonya