.

1/12/2019

Jitibu ugonjwa wa sikio kwa kutumia kitunguu Maji


Sikio, pua na koo ni viungo vinavyohusiana kwa ukaribu sana kiasi kwamba linapotokea tatizo katika kiungo kimoja wapo, tatizo hilo pia huweza kujitokeza pia katika kiungo kingine.

Mfano inapotokea pua zimeziba, basi masikio pia yanaziba au sikio linapouma pia pua huweza kutoa kamasi hali kadhalika na koo linapouma wakati wa kumeza chakula sikio pia linauma.

Miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha maumivu ya sikio pamoja na uwepo wa jipu au upele ndani ya njia, kelele za nguvu, kupenga kamasi kwa nguvu, kukaukiana kwa nta ndani ya sikio. Mara nyingi maumivu mengi ya sikio huwa yanakubali matibabu kwa urahisi.

Zipo tiba mbalimbali za sikio linapokuwa na maumivu, lakini kwa leo nitakufahamisha hii ya kutumia kitunguu maji ambacho ni rahisi hata kukipata katika mazingira yetu ya kila siku.

Unachopaswa kufanya ili kukamilisha tiba hii ni kuchukua kitunguu maji kisha tengeneza juisi yake na baadaye utatumia matone 3-5 katika sikio. Fanya hivyo, mara 3 kwa siku kwa muda wa siku 5, Tiba hii ni mahususi kwa sikio linalouma au ambalo limeziba kutokana na kujaa nta.

Ukiona hakuna dalili zozote za kupona tafadhali nenda hospitali ukamuone daktari kwa ushauri zaidi.

Na. Benson Chonya