https://monetag.com/?ref_id=TTIb Kevin Prince Boateng kuongeza nguvu Barcelona | Muungwana BLOG

Kevin Prince Boateng kuongeza nguvu Barcelona


Klabu ya Barcelona imemsajili kiungo Kevin Prince Boateng kutoka Sassoulo kwa mkataba wa awali wa mkopo mpaka mwisho wa msimu huku kukiwa na chaguo la kumnunua mwisho wa msimu huu.

 Kevin Prince Boateng anakuja kuongeza nguvu katika kikosi cha Barcelona ambacho kinaongoza ligi nchini Hispania (Laliga) wakiwa tayari wamejikusanyia pointi 46 katika michezo 20 waliocheza, huku wakifatiwa na mahasimu wao wa karibu Atletico Madrid ambao wana pointi 41.