Maagizo mazito ya RC Mwanri kwa Mkandarasi (+video)


Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri imemwagiza Mkandarasi wa L and T kufanyia marekebisho ya kasoro na udhaifu uliojitokeza katika utekelezaji wa ujenzi wa tenki la maji la ujazo lita milioni moja uliokuwa ukijengwa katika Kijiji cha Ibelamilundi wilayani Uyui baada ya Kamati iliyoundwa kubaini baadhi ya mapungufu kwenye maendeleo ya mradi huo.

Ametoa maagizo hayo hiyo baada ya kupokea taarifa ya Kamati aliyokuwa ameiunda kuchunguza ubora wa kazi katika ujenzi wa hilo kubaini uwepo wa kasoro katika usukaji wa nondo na Mkandarasi kutumia michoro ambayo hajaidhinishwa na Mshauri wa Mkandarasi.

Pia Kamati imebaini udhaifu katika usimamizi wa Mhandisi Mshauri (Consultant ) mradi huo ikiwemo na ule upande wa Serikali kutotembelea mradi na kutoa ushauri wa kuboresha kasoro na kutokuwa na mawasiliano ya karibu wakati wa ujenzi wa mradi huo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI, PIA SUBSCRIBE