.

1/12/2019

Maimartha atoa somo kupitia Wema Sepetu na DiamondMtangazaji/ MC, Maimatha Jesse amefunguka juu ya mpango mzima wa mahusiano ya Kimapenzi kwa kumlenga msanii wa Filamu , Wema Sepetu na Diamond Platnumz waliowahi kuwa kwenye mahusiano miaka kadhaa.


Maimartha ameandika hivi kwenye mtandao wake wa Instagram; "Kweli wanawake tuna huruma saanaa.Hii ni Enzi hizo, Jamani wema alimpenda Nassib.....tena akiwa hana chochote maskini....kama unavyoona pichani, Dah watu wanatokaga mbali wallahy."

Aliendelea kuandika hivi; "Nakumbuka warembo wa mujini walikuwa wanamshangaa wema wanamwambia kwanza anatembeaje na kijana asiye type yake.Hana muonekano, hamuendani wema akawa kimya."

Aliongeza kuwa "Hata siku Mimi nilivyoambiwa I was like oops..love don't ask why Alimvalisha......alimpa promo ...bwana Nassib taratibu akaanza kujulikana kwa kuongeza juhudi zake kwa kujituma .Oh kweli sasahivi ni moto wa kuotea mbali...Nassib anamaendeleo kama yote..... Pesa ndefu.Umejifunza nini."

Miaka kadhaa iliyopita msanii Diamond alikuwa kwenye mahusiano na mrembo, Wema Sepetu na waliachana ambapo mpaka sasa Diamond yupo katika mahusiano mengine.