https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mambo mawili (2) yatakayokuepusha na usingizi wakati wa kujisomea | Muungwana BLOG

Mambo mawili (2) yatakayokuepusha na usingizi wakati wa kujisomea

Asante kwa kutuchagua sisi Muungwana blog kama sehemu sahihi ya kupata elimu mbalimbali, naomba nichukue nafsi hii kukuarika rasmi ili tuweze kujifunza mambo mawili ya msingi yatakayotusaidia kuepekana na usingizi wakati wa kujisomea.

Kumekuwako na changamoto nyingi zinajitokeza wakati wa kujisomea na miongoni mwa sababu zinazochangia ni pamoja na usingizi.

Zifutazo ndizo sababu mbili zinazopelekea watu kupatwa na usingizi wa kujisomea na jinsi ya kuziepeka.

1. Chakula.
Ili kuepukana na usingizi unashauriwa kuchagua chakula sahihi kwa kwako, chakula ambacho hakitaleta usumbufu wa tumbo mara baada ya kula. Kama kuna chakula fulani huwa kinakusumbua ukila tafadhari epukana na chakula hicho kabla ya kuanza kujisomea kwani pindi utakapoamua kula chakula hicho utashindwa kusoma vizuri.

Pia kwa upande mwingine unashauriwa kuwa mtu akila huwa anakuwa mvivu sana, kama itawezekana ni heri usile chakula ila mara baada ya kusoma ndiyo utakula chakula hicho, au ukishindwa kufanya hivyo basi unashauriwa ule chakula kwa kiwango kidogo sana kwa sababu upo usemi usemao shibe ni mwana malevya.

Hivyo ni ushauri wangu wa  dhati kwako kuwa kama utashindwa kutokula, kula kiasi kabla ya kuanza kusoma basi mara baada ya kula chakula unatakiwa kupumzika walau nusu saa ndipo uanze kujisomea tena, kwani pindi ukimaua kula na kuanza kujisomea ni lazima utalala tu maana wakati huo chakula nacho kitataka kifanye kazi katika mwili wako.

2. Eneo la kujisomea.
Wakati mwingine utakuwa unashangaa ni kwanini kila ukianza kusoma usingizi huwa unakunyemelea? wala usipate tabu nipo hapa kwa ajili yako, ujue upi hivi wakati wa kujisomea ni suala nyeti sana, hivyo unatakiwa kukaa eneo tulivu na lisilokusababishia wewe kupatwa na  usingizi.

Kwa mfano wapo baadhi ya watu hupenda kusoma wakiwa wameketi kitandani, hebu jiuluze kwa mtindo kama huu na mazingira kama haya unadhani hautalala kweli? Bila shaka ni lazima utalala tu hata iweje.

Hivyo  ili usiweze kusinzia wakati wa kujisomea unashauriwa kukaa mbali na mazingira ambayo huwa unalala kama vile chumbani, hosteli na sehemu zingine kama hizo.

Ukienda kwenye shule zenye hosteli huwa kuna utaratibu wa wanafunzi kujisome nyakati za usiku wao huita (prepo), hivi unadhani wangewambia wanafunzi wawe wanajisomea wao wenyewe huko huko mabwenini kwenye mazingira ya kulala ni wanafunzi wangapi wangekuwa wanajisomea? Majibu hayo baki nayo.

Hayo ni mambo ya msingi ya kuyaepeka ili usipatwe na usingizi wakati wa kujisomea, ukizingatia hayo utasoma vizuri, msuli utakuwa tembo na matokeo pia yatakauwa tembo.

Na: Benson Chonya