Mbunge CHADEMA aingilia kati sakata la CAG na Spika Ndugai


Mbunge Viti Maaalum CHADEMA na Waziri Kivuli wa Nishati, Jesca Kishoa amemshauri Spika wa Bunge kumuita mbele ya kamati ya bunge ya maadili Mwanasheria mkuu wa Serikali kwa kulidanganya Bunge na kushindwa kufanyia kazi taarifa za Ufisadi unaendelea katika mikataba ya kampuni ya kuzalisha Umeme wa Gesi ya SONGAS badala ya kumuita CAG Profesa Assad kwa kusema maneno ya ukweli.

Kishoa anatoa Rai hiyo jijini Dodoma ambapo amesema Ufisadi huo Unaendelea umebainishwa katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2009 na ya mwaka 2018 ambapo mwanasheria mkuu wa serikali aliahidi mbele ya Bunge kua atalifanyia kazi ambapo mpaka sasa hajalifanyia kazi huku Bunge likishindwa kumuwajibisha.

Katika Ripoti hizo za CAG zilionyesha Tanzania mepoteza zaidi ya Tsh. 1.3 na mikataba hiyo ikiendelea itapoteza zaidi hivyo, pia  ameomba Rais Magufuli kutumia Mahakama za Kimataifa katika swala hilo kama kwake limekua gumu.