.

1/10/2019

Mchezaji Kamusoko wa Yanga ajiengua rasmi kwenye timu


Mchezaji wa klabu ya Yanga, Mzibambwe, Thaban Kamusoko, ameamua kuachana rasmi na Klabu hiyo.

Mchezaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika akiwashukuru wadau na mashabiki wa timu hiyo kwa muda wote aliokaa na timu.

"Katika kukaa kwangu hapa Yanga, nimejifunza vitu vingi , nilikuja Yanga na nilijifunza vile watu wanathamini pale unapoonesha kujitolea katika timu.

Pia Kamusoko amesema anawashukuru mashabiki wote kwa mapenzi waliompa na ambayo bado wanampa na anathamini sana.