Mchezaji wa Yanga SC aliyefiwa apewa pole


Uongozi wa Yanga SC, umetoa pole kwa kipa wa timu hiyo Klaus Kindoki  ambaye amepatwa na msiba wa kufiwa na baba yake mzani huko kwao DR Congo.

Taarifa zinasema msiba huo utafanyika kwao DR Congo ambapo mazishi yatafanyika Jumapili ya wiki hii.

Kindoki amepatwa na msiba huo akiwa Shinyanga ambapo Yanga inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kesho.