Mose Iyobo afunguka kuachana na Aunt Ezekiel, amgusia Diamond


Dansa wa msanii Diamond Platnumz, Mose Iyobo ametupilia mbali tuhuma za yeye kulelewa na mzazi mwenzie, Aunt Ezikiel.

Hivi karibuni kuliibuka taarifa za Aunt Ezekiel kuachana na Mose Iyobo kitu ambacho amekikanusha vikali.

"Nalelewaje wakati nafanya kazi kwa Diamond, nikimwambia Diamond nataka gari fulani inachukua dakika chache sana," amesema Iyobo akihojiwa na Wasafi TV.

Ameendelea kwa kusema, "Diamond ni mtu fulani yupo poa sana, siwezi kusema nitoka pale (WCB) niende sehemu nyingine, labda nikafungue kitu changu mwenyewe,'.