Msuva atoa somo kwa Simba kuhusu Waarabu


Mtanzania Simon Msuva anayecheza katika klabu ya Difaa El Jadid ya Morocco, ametoa somo kwa kikosi cha Simba juu ya mbinu za waarabu uwanjani.

Imeelezwa Msuva ameibuka na kufunguka kuwa ni kweli waarabu wana mbinu za kujiangusha lakini vilevile ni wapambanaji ndani ya Uwanja.

Msuva amewashauri Simba kujipanga zaidi kutumia vema Uwanja wa nyumbani ikiwemo kufunga mabao ya mapema ili kutoa mwangaza mzuri kwao na mgumu kwa wapinzani.

Kauli ya Msuva imekuja kutokana na kundi D ambalo lina timu za AS Vital, Alh Ahly na JS Saoura ambazo zote ni moto wa kuotea mbali.

Ameeleza kuwa waarabu hupoteza muda kwa kujiangusha ovyo-ovyo kama mbinu yao ya kupoteza muda, hivyo ni jukumu la Simba kuwapa ugumu wa kufanya hivyo.