https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mwenyekiti wa CCM ashusha neema Tarime | Muungwana BLOG

Mwenyekiti wa CCM ashusha neema Tarime


Na.  Clonel Mwegendao Tarime

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Tarime Mkoani  Mara Daud Marwa Ngicho ametoa kiasi cha shilingi Millioni Moja, Mifuko 50 ya Saruji na  Tripu 05  za Mchanga kwa ajili ya kuunga nguvu za wananchi katika ujenzi wa shule ya msingi Keweirumbe iliyopo katika kijiji cha Masurura kata ya Goronga Wilayani Tarime Mkoani Mara  ili kupunguzia wanafunzi hao kutembea zaidi ya Kilometa 600.

Mwenyekiti huyo alidai kuwa ameamua kuchangia Ujenzi huo baada ya kuona nguvu za wananchi katika ujenzi huo kuwa kubwa na kuonyesha nia na moyo wa kuchngia  kwa lengo la kuwapunguzia watoto umbali mrefu wanaotembea kufuata masomo katika shule ya Msingi Masurura au Kitawasi.

“Nimetoa vifaa hivi kuunga mkono nguvu za wananchi nimetoa Millioni Moja, Mifuko 50 ya Saruji,Tripu 05 za mchanga pamoja na Gari la kuleta vifaa hivi mpaka eneo la ujenzi” alisema Ngicho.

Watoto hutembea umbali takribani km 600 kufuata shule Jambo ambalo hupelekea baadhi ya watoto kushindwa kujiunga na elimu ya msingi huku baadhi ya wazazi wakidai  suala hilo namba inazidi kuwa kubwa ya watoto wasijua kusoma na kuandika.

 Aidha shule hiyo yenye madarasa mawili pamoja na nyumba moja ya mwalimu Ina jumla ya wanafunzi wa awali 88 wanaoingia darasa la Kwanza sasa inatarajia kupokea wanafunzi 150 mwaka huu ambapo  licha ya kuwepo mapungufu katika shule hiyo wazazi wamedai hawana sehemu nyingine ya kuwapeleka kutokana na umbali uliopo kufikia shule nyingine hivyo wameiomba serikali pia kuwaunga mono katika ujenzi huo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Tarime Godfrey Fransis aliwapongeza Wananchi hao kwa kujitoa katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kupunguzia wanafunzi hao umbali mkubwa  wanaotembea.