Neno la Isha Mashauzi kwa Mzee Yusuph baada ya kuacha Taarabu ' Kuna kukurupuka'


Msanii Mkongwe wa Taarabu, Isha Mashauzi, amefunguka kwa mara ya kwanza tangu Alhaj Mzee Yusuph kuacha kufanya muziki huo.

Mashauzi amesema kuwa Mzee Yusuph yeye aliamua kuacha taarabu hakukurupuka na aliamua muda mrefu na akafanya kitu ambacho ni sahihi kwake.

"Unajua siku zote usifanye kitu kwa kuiga, nisikuone wewe mtangazaji na mimi nikaanza kukuiga kwahiyo ni vitu viwili tofauti, kuna kukurupuka na kuamua, Mzee Yusuph yeye aliamua hakukurupuka kwahiyo naamini aliamua muda mrefu na akafanya kitu ambacho ni sahihi kwake na sisi tunamuombea Mungu," alisema Isha mashauzi.

Mwaka uliopita Mzee Yusuph alimua kuachana na muziki wa  aina hiyo na kumrudia Mungu, Ambapo kwasasa anafanya biashara ya matofali Chanika jijini Dar Es salaam.