Ngassa apatwa na pigo


Mrisho Khalfan Ngassa ambaye ni Mshambuliaji wa timu ya Yanga SC, amepata pigo la kuondokewa na baba yake mdogo ambaye amefariki leo Jumamosi huku chanzo cha kifo hicho kikiwa hakijaelezwa.

Kupitia katika mtandao wake wa kijamii wa instagram, Ngasa ameandika ujumbe unaosema
“Pumzika kwa amani baba yangu mcheshi wangu mtani wangu leo hii umetutoka baba R.I.P”

Wakati Ngassa akipata pigo hilo mlimda mlango wa timu hiyo Klaus Kindoki naye Baba yake Mzee Kindoki Nkinzi anatarajiwa kuzikwa Leo huko kwao DR Congo.