.

1/14/2019

Ombi la Vanessa Mdee kwa mashabiki wake


Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amezidi kuwasisitiza mashabiki wake kumpigia kura kwenye tuzo za Hi Pipo Music Awards kutoka nchini Uganda.

Vanessa anawania vipengele sita kwenye tuzo hizo, miongoni mwa vipengele anavyowania ni pamoja na msanii Bora wa Kike Afrika Mashari na Video ya Mwaka kutoka Tanzania kupitia wimbo wake uitwao Wet.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa March 16 mwaka huu Kampala Uganda kwenye Hoteli ya Serena. Wasanii kutoka mataifa ya Ghana, Nigeria, Afrika Kusini, Kenya na kwingineko wanatarajiwa kushiriki.