Picha: Mkataba ubanguaji korosho wasaniwa, Tani 7,500 kubanguliwa


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba ya ubanguaji korosho kati ya Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania na wenye viwanda vya ndani.

Mkurugenzi wa Bodi ya nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dkt Hussein Mansoor ndiye ametia saini kwa niaba ya serikali na Kampuni nne zimesaini mikataba ya awali kuanza kazi hiyo ambazo ni kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd, Micronix Mtwara, Korosho Afrika, na Micronix-Newala.
Kampuni hizo zimeingia mikataba ya Jumla ya Tani 7500 ambapo kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd yenye uwezo wa kubangua Tani 2000 kwa mwaka imesaini mkataba wa Tani 1500.

Kampuni ya Micronix ya mjini Mtwara imeingia mkataba wa Tani 1200. Kampuni ya Korosho Afrika ya Mjini Tunduru Mkaoni Ruvuma imeingia mkataba wa kubangua Tani 2400, huku Kampuni ya Micronix ya Wilayani Newala imeingia mkataba wa kubangua Tani 2400.