.

1/10/2019

Pongezi za Bilionea Mo Dewji kwa Mbwana Samatta


Mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ambaye pia ni mwekezaji ndani ya timu ya Simba SC amempongeza Mbwana Samatta kuwa mchezaji bora nchini Belgium.

Utakumbuka kabla ya Mbwana Samatta kutimukia TP Mazembe alikuwa mchezaji wa Simba SC. Kupitia ukurasa wake wa twitter MO ameandika;

"Hongera Mbwana Samatta kwa kuongoza orodha ya wafungaji bora nchini Belgium, muda wote unafanya Watanzania kujivunia wewe," ameeleza MO. 

Mbwana Samatta kwa sasa anaichezea KRC Genk inayoshiriki ligi kuu  Belgium. kwa mujibu wa jarida maarufu la masuala ya fedha la Forbes linaeleza kuwa utajiri wa wa kijana huyu kufikia US Dollar Bilioni 1.5.