.

1/14/2019

Rais Trump atuma ujumbe wa vitisho Uturuki kisa Syria


Rais wa Marekani, Donald Trump umetuma ujumbe vitisho kwa Uturuki iwapo taifa hilo litawashambuliwa vikosi vya wakurdi nchini Syria.

Trump ameeleza itaiangamiza Uturuki kiuchumi, ikiwa ni baada tu ya wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini Syria.

Kupitia mtandao wa Twitter Rais Trump amechapisha ujumbe na kueleza kuwa hakutaka Wakurdi kwa upande wao nao pia waichokoze Uturuki.

Kauli ya Rais Trump inafuata mara baada ya uamuzi wake wa ghafla kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Syria. Vikosi vya Marekani vilikuwa vikipambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS).