Loading...

1/14/2019

Taarifa kuhusu Polisi kupigana na Dereva


Jeshi la Polisi limezungumzia kitendo cha Polisi wa usalama barabarani kuonekana akipigana na dereva.

Kaimu Kamanda wa Polisi Songwe amesema kuwa dereva hakupingwa bali polisi wakitaka kumdhibiti mara baada ya kusimamishwa na kukaidi amri.

"Dereva hakupigwa ilikuwa katika harakati za kumdhibiti na kwa sababu alikuwa anatumia nguvu ndo maana Askari walitumia reasonable force, hakupigwa ila alikuwa anadhibitiwa ili tuweze kumkamata afikishwe katika Vyombo vya Sheria," amesema.

Ameendelea kwa kusema dereva huyo alisimamishwa na kutoa kashfa na kuondoka ndipo walipomfuatilia na kumkamatia Tunduma ambapo alianza kumshambulia Askari na wao walitumia nguvu za kadri kwa lengo la kumthibiti.

Loading...