.

1/12/2019

Tabora yakabiliwa na upungufu wa madarasa 250Na. Rahel Nyabali, Tabora.

Wanafunzi zaidi ya 16,000 ambao wanaingia  kidato cha  kwanza  mwaka  huu  mkoani Tabora  wanakabiliwa na upungufu  wa  vyumba  vya  madarasa  zaidi  ya  250.

Ilikuweza kukizi ongezeko la  huku  asilimia  sabini  na tano ya wanafunzi  elfu  kumi  na moja  watoro  sugu  na  rejareja   waliojaribu  kuacha  masomo  wamerejea  tena shuleni  na hivyo  ongezeko  hilo limesababisha kuwepo  kwa  upungufu  mkubwa  wa  vyumba  vya  madarasa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa huu,  Agrey Mwanri katika Kikao  kinachowakutanisha  viongozi  wa  Serikali na viongozi  wa  Chama  cha Walimu (CWT)  Mkoa  wa  Tabora  kikiwa  na  malengo  ya  kujadili  hali  ya  maboresho  ya  Elimu  kwa  shule za  Msingi  na  Sekondari,Suala  la  upungufu  wa  Vyumba  vya  Madarasa  linapewa  kipaumbele.

Hata hivyo, Suala la nidhamu ya walimu na  wanafunzi,pamoja  na chakula  shuleni  ni  mambo  mengine  yaliyochukua  nafasi  katika  majadiliano ndani  ya  kikao hicho ikiwa ni lengo la kuinua sekta ya Elim.

 Aidha CWT Mkoa wa Tabora kimeihakikishia Serikali kushilikiana nayo katika  kutekeleza wajibu na  majukumu waliopewa walimu maeneo yao ya kazi huku ikilipa ikienda kinyume na  suala  la  migomo  ambayo  lilikuwa likijitokeza hapo awali wakati  wa  kudai  haki  stahili za  walimu  kwa  mwajiri.