Tsh. Trilioni 1.3 kutatua shida ya maji katika miji 28


Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amesema serikali inatarajia kutumia Tsh. Tirioni 1.3 kupitia mkopo toka Exim benki ya nchini India kwa ajili ya miradi mikakati ya maji katika Miji 28nchi nzima.

Amebainisha hayo alipofanya ziara katika mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini
Tanga(Tanga-Uwasa) na kuzungumza n watumishi wake.

Amesema katika fedha hizo zaidi ya TSh. Bilioni 140 zitainufaisha Miji ya Pangani,Muheza na Korogwe ambapo matarajio ya Serikali kuhakikisha kufikia malengo ya asilimia 85 Vijijini na 95 Mijini hadi kufikia 2025.

katikaMiji hiyo Pangani imepangiwa kiasi cha Tsh. Bilioni 22.5,Muheza Bilioni 5.6 na Korogwe kupitia mradi Mkuu wa maji Korogwe na Handeni Bil. 112.5.