.

1/14/2019

Tundu Lissu aanza ziara Uingereza, kisha Marekani


Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki
yupo nchini Uingereza katika ziara yake ya barani Ulaya.

Mwanasheria huyo Mkuu wa CHADEMA anatarajia kutumia ziara yake hiyo kueleza tukio la kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Utakumbuka Septemba 17, 2017 Tundu Lissu alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa risasi
akitokea Bungeni Jijini Dodoma. Lissu alipatiwa matibabu ya mwanzo nchini Kenya kisha kuhamishiwa Ubelgiji.