.

1/12/2019

Vitambulisho vya Rais Magufuli vyawa gumzo Dodoma


Vitambulisho vilivyotolewa na Rais Dk John Magufuli kwa wafanyabiashara wadogo wadogo ‘machinga’ vimezua gumzo jijini Dodoma baada ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi kuvigawa.

DC Katambi amezindua ugawaji wa vitambulisho 500 kwa kuanza na wafanyabiashara 100 kama wawakilishi ambapo amewataka kufanya kazi kwa bidii ili kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuiletea maendeleo Tanzania.

“Serikali inatambua wapo watu wengi waliojiri na kwa kuzingatia hilo Mhe. Rais Magufuli akaona sasa ni vizuri aandae utaratibu rasmi wa kuwatambua wafanyabiashara wote wadogo, hivyo tufanyeni kazi ili tusimuangushe Rais wetu mpendwa.

“Kwahiyo kwa Jiji letu LA Dodoma, ni marufuku baada ya muda tuliojipangia kufanya biashara katika jiji letu bila kuwa na kitambulisho hiki ambacho Mhe. Rais Magufuli kakitoa kwa upendo mkubwa,” amesema DC Katambi.

Wafanyabiashara hao wamemshukuru Rais Magufuli kwa upendo aliouonesha kwa kuwathamini na kuwapa kipaumbele huku wakimsifu DC Katambi na Mkurugenzi wa Jiji kwa utaratibu bora walioupanga katika kuhakikisha kila machinga anapata vitambulisho hicho