Wahamiaji kutoka katika baadhi ya mataifa ya Amerika Kusini wameanza kuwasili mpakani mwa Marekani na Mexico huku wengine wakiripotiwa kuomba hifadhi mpakani mwa Guatemala na Mexico, baada ya kuomba hifadhi wahamiaji hao huendelea na safari yao ambayo malengo yao ni kuingia nchini Marekani.
Uongozi wa shirika la kutetea haki za wahamiaji INM umeomba kuondolewa na vikosi vya usalama kwa lengo la kuzuia kutokea ghasia baina yao na wahamiaji.
Mexico imeongeza idadi ya maafisa wa idara ya uahamiaji katika mpaka wake wa Kusini kwa lengo la kuzuia msongamano wa mwahamiaji mpakani. Taarifa ziznafahamisha kwamba wahamiaji wanaoingia Mexico kutoka Amerika Kusini watapewa hifadhi katika kambi ya Suchiate.
Idara ya uhamiaji ya Guatemala amefahamisha kuwa raia takriban 700 kutoka Honduras na 107 kutoka El Salvador wamevuka mpaka wakiwa katika safari yao kuelekea nchini Marekani.