https://monetag.com/?ref_id=TTIb Wambura kukata rufaa ya FIFA | Muungwana BLOG

Wambura kukata rufaa ya FIFA


Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Richard Wambura amepinga uamuzi wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kumfungia maisha na kusema kuwa  bodi hiyo ya soka duniani imemuhukumu kwa taarifa potofu.

Kupitia kwa Mwanasheria wake, Emmanuel Muga, Wambura amesema kwamba FIFA ilipelekewa taarifa potofu na TFF juu ya mteja wake hivyo imemuhukumu kimakosa.

Kamati ya nidhamu ya FIFA chini ya Mwenyekiti wake, Anin Yeboah wa Ghana imekazia hukumu ya Kamati ya Maadili ya TFF kumfungia maisha Wambura kujihusisha na soka iliyotolewa Aprili 6 mwaka jana.

Lakini Muga amesema kwamba watakata rufaa FIFA ndani ya siku 10 walizopewa kuhakikisha wanapata haki yao na hawana shaka mwisho wa misukosuko yao umewadia.