Wanafunzi 235 wapewa Mimba, madereva bodaboda wapewa onyo kali


Inaarifiwa kuwa kwa kipindi cha mwaka 2018 Wanafunzi wa kike 235 wa shule za msingi na sekondari mkoani Pwani wamepewa mimba.

Hayo yamebanishwa na ofisa elimu mkoa wa Pwani, Abdul Maulid ambapo amesema kati ya wanafunzi hao, 155 ni wanafunzi wa shule za sekondari, huku 80 wakiwa wa shule za msingi.

“Mikoa ya wenzetu kama Kilimanjaro tujiulize kwanini wanafunzi hawapati mimba ,tushirikiane kupiga Vita tatizo hili," amesema.

Aliendelea kwa kusisitiza, 'Madereva bodaboda, jamii ishirikiane na serikali kupambana na namba hii, bodaboda msiwe chanzo cha kupakia wanafunzi hawa na kuwarubuni,'.