Waziri Mhagama atema cheche, 'Hatutakuwa na msamaha kwa wazembe'



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameridhishwa na utendaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa umma wa PSSSF Mkoani Singida, huku akisitiza kutokuwa na msamaha kwa watendaji wazembe.

Hayo yamebainishwa wakati wa ziara yake mkoani humu alipokuwa akizungumza na viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA), viongozi wa vyama vya waajiri, Watendaji wa Wizara inayohusika na Mifuko ya hifadhi ya jamii.

“Nimetembelea mifuko hii miwili na kuridhishwa na utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais ikiwa tayari wa wastaafu 89 kati ya 143 wameshaanza kufanyiwa uhakiki tangu utekelezaji wake ulipoanza wiki hii”,alisema Mhagama.

Aliendelea na kuongeza kuwa “Hatutakuwa na msamaha na watendaji wazembe katika kutekeleza maagizo hayo, lazima utekelezaji wake uwe kwa wakati na watakaozembea watachukuliwa hatua za kisheria”,alisisitiza Mhagama,".