.

1/09/2019

Yanga Leo kucheza mechi ya mwisho Kombe la Mapinduzi


Kikosi cha Yanga Leo kitacheza mechi ya mwisho ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Pemba, kisha itapanda boti na kurejea Dar kutokana na kutokuwa na chake kwenye michuano hiyo.

Yanga na Jamhuri zitacheza mechi hiyo ya Kundi B kwenye Uwanja wa Amaan kuanzia saa kumi jioni.

Yanga katika michuano hiyo imeshindwa kufanya vizuri kutokana na kucheza mechi tatu na kujikusanyia pointi tatu baada ya kushinda moja na kufungwa mbili.

Katika kundi hilo, Azam inaongoza ikiwa na pointi saba sawa na Malindi ambazo zote zimefuzu nusu fainali. Jamhuri ina pointi nne, Yanga (3) na KVZ inaburuza mkia na pointi moja.