.

1/14/2019

Yanga Princess waeleza kilichopelekea kufungwa 7-0 na Simba Queens


Hapo jana michezo ya Ligi ya Wanawake iliendelea ambapo mchezo uliovuta hisia za wengi ni ule
uliowakutanisha Yanga Princess na Simba Queens.

Katika mchezo huo timu ya Yanga Princess ilijikuta ikishushiwa kichapo kizito cha goli 7 kwa bila kutoka kwa Simba Queens.

Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Maalim Saleh amesema kuwa timu yake imepoteza mchezo huo kutokana na wachezaji wake kukosa uzoefu wa kutosha ukilinganisha na wapinzani wao.

"Simba walikuwa na uzoefu mkubwa sana hata ukiangalia kwa mchezaji mmoja mmoja lakini
tutajipanga ili tuweze kupata timu bora," amesema.

Kwa matokea hayo Simba Queens wanafikisha pointi 13 na kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, huku Yanga Princess wakikamata nafasi ya saba na pointi zao sita kibindoni.