Account ya Marehemu Godzilla yadukuliwa na kufanywa page ya umbea



Tangu siku kadhaa zipite, Tangu Msanii wa Muziki, Golden Mbunda (Godzilla) apumzishwe kwenye nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kindondoni jijini Dar Es Salaam, Leo jambo lililostahajabisha lni kitendo cha akaunti yake ya Instagram kua-hacked account na kufanywa page ya umbea.

Msanii wa Hip Hop, Fareed Kubanda, Fid Q ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa taarifa kuwa account aliyokuwa akiitumia Godzilla imechukuliwa na sasa inamilikiwa na Umbea Queen huku akionyeshwa kusikitishwa na kitendo hicho.

“Daaah.. Yaani hatujafikisha hata wiki tangu tumpumzishe ndugu yetu kwenye makazi yake ya milele.. HACKERS washapita na page ya insta ya ZIZI..!!?