.

2/12/2019

ALAT watekeleza agizo la Rais Magufuli


Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) imeunga mkono agizo la Rais John Magufuli lililotaka Taasisi zote kuhamia Makao Makuu ya Nchi kwa kuanza ujenzi wa Jengo la Kitega uchumi Jijini Dodoma.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea Jengo dogo linaloendelea kujengwa hivi sasa  Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Gullam Hafeez Mukadam amesema wameanza na kujenga jengo dogo kwa ajili ya Ofisi ambalo litakamilika mwishoni mwa mwezi huu.

“Kama mnavyoona hapa ujenzi unaendelea na tumeamua kuanza kwa kujenga jengo dogo la Utawala ambalo litatumiwa na watumishi na viongozi wote wa ALAT na eneo linalobakia ndio ambalo litajengwa Jengo la Kitegauchumi” alisema Mukadam.

Aliongeza kuwa kiwanja hiki kina ukubwa wa zaidi  Square meter 6000 na hili jengo linalojengwa sasa linatumia takribani Sqm 1000 tu hivyo eneo lililobakia ni kubwa na litatosha kwa ajili ya mradi wetu wa kitega uchumi tunaoutarajia.