Asakwa na Polisi kwa tuhuma za kumbaka Bibi Kizee hadi kufa


Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamsaka kijana William Saimon kwa tuhuma za kumbaka Bibi Kizee Jema Macheho (77).

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani humo, Gilles Muroto amesema bibi huyo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.

Katika hatua nyingine jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa hati za viwanja, kubadili ramani za mpango mji na kuuza viwanja kwa njia ya utapeli.