Asije akarogwa kiongozi wa serikalini akauliza swali tutamzibua - RC Mwanri


Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amewakemea Viongozi wa Serikali katika Mkoa wake wanaopotosha tafsiri ya vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo hii ni baada ya baadhi ya viongozi kupinga zoezi hilo.

RC Mwanri amema kuwa kiongozi yoyote asiposimama kwenye nafasi yake na kuelezea vyena maagizo ya serikali watamtazama kwa jicho la dharau na bila heshima

"Ndio maana nimeruhusu watu waongee hapa, asije akarogwa kiongozi wa serikalini akauliza swali hapa tutamzibua hapo hapo ndio maana nawaambia hoja hii imeletwa na serikali alafu wewe unapinga maana yake nini?," alisema na kuhoji RC Mwanri.