.

2/12/2019

Baada ya 'Kukatika' na Diamond, Navy Kenzo watangaza vita nyingine


Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo limetangaza ujio wa ngoma yao mpya mara baada ya kufanya vizuri na 'Katika' waliyomshirikisha Diamond Platnumz.

Msanii wa kundi hilo ambaye pia ni prodyuza, Nahreel ameeleza kuwa wimbo huo mpya utakwenda kwa jina la Roll it na utatoka rasmi wiki ijayo.

Utakumbuka wimbo hao katika uliweza kufanya vizuri hadi kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za muziki za BBC Radio 1Xtra nchini Uingereza.

Ukiachana na hilo, Navy Kenzo wamedokeza pia ujio wa albamu yao mpya ya pili itakayokwenda kwa jina la Temperature baada ya ile ya kwanza, Above In A Minute (AIM).