.

2/10/2019

Binti mfalme wa Thailand aondolewa kwenye kinyang'anyiro cha Uwaziri mkuu


Binti mfalme wa Thailand Ubolratana ameondolewa katika kinyang'anyiro cha kugombea uwaziri mkuu wa taifa hilo na chama alichokuwa akikiwakilisha. Maamuzi hayo yameyafanywa baada kupokea  onyo la Mfalme.

Taarifa ambayo imetolewa na chama ambacho binti mfalme huyo angekiwakilisha kwenye uchaguzi, chama cha Thai Raksa Chart inasema wametii pingamizi la mfalme hivyo binti mfalme huyo hatokiwakilisha tena chama hicho.

Mara baada ya mfalme wa Thailand Vajiralongkorn mwenye umri wa miaka 67, mara baada ya kutangazwa kwamba dada yake binti mfalme Ubolratana Rajakanya Sirivadhana Barnavadi kuwa mgombea wa nafasi ya waziri mkuu alisema suala hilo ni kinyume na taratibu za nchi hio kwani wanafamilia ya mfalme hawaruhusiwi kujihusisha na siasa.

Binti mfalme naye muda mchache baada ya taarifa ya mfalme bila kuzungumzia suala la ugombeaji wake aliwashukuru watu wa Thailand kwa ushirikiano waliomuonyesha.

Thayland itafanya uchaguzi kwa mara ya kwanza tangu baada ya mapinduzi ya mwaka 2014.