Dkt. Mwigulu aruhusiwa kutoka hospitalini, atoa neno kwa Watanzania


Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Dkt. Mwigulu Nchemba aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo.


Dkt. Mwigulu Nchemba kwenye ukurasa wake wa Twitter leo ameandika "Nashukuru Mungu nimeruhusiwa kutoka Hospitali, Shukran kwa mhe Rais na wasaidizi wake wote kwakuwa karibu nami,wabunge,viongozi wa Chama na Serikali, madaktari kwa matibabu ya haraka, wananchi wote kwa maombi yenu na salamu za kunitakia heri."

"Zaidi namshukuru Mungu kwa yote," aliongeza.

Ikumbukwe, Dkt. Mwiguli alipata ajali Februari 13, 2019 katika eneo la Migori mkoani Iringa akitokea mkoani humo kwenda mkoani Singida baada ya gari lake kugonga punda waliokuwa wanakatisha barabara.