Dudu Baya kufunga ndoa mwaka huu


Msanii  mkongwe wa Bongo Fleva, Dudu Baya ameweka wazi kuwa moja ya mipango yake ni kufunga ndoa mwaka huu.

Dudu Baya ameeleza hilo mara baada ya kusikia wimbo mpya wa Linex na Lady Jaydee uitwao Too
Late.

"Hii ngoma siwezi kulala bila kuisikiliza mara 10, inanifundisha watu wengi hujua umuhimu wa mtu
akiondoka. Na mwaka huuu navyotaka kufunga ndoa ni somo tosha kwangu," ameeleza Dudu Baya kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Utakumbuka kuwa hadi sasa Dudu Baya ni baba wa watoto wawili. Kwa wakati huu anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Konki aliyomshirikisha Rayvanny kutokea WCB.