Jamii yatakiwa kuacha Siasa kwenye maendeleo


Na Timothy Itembe.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, Elias Ntiruhungwa alisema jana katika kikao cha kutambulisha mradi wa kisasa wa ujenzi wa Soko kuu unaotarajiwa kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Ntiruhungwa alisema kuwa moja ya mambo ambayo jamii inatakiwa kuyaepuka ni kuingiza siasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa jamii inayokuwa inatekelezwa.

Mkurugenzi huyo alitoa miezi mitatu kwa wafanyabiashara hao ili kujiandaa kuhama ifikapo mwezi wa Tano mwaka 2019 na kuwa kwa atakaye kuwa na rasilimali yake ndani ya Kibanda atapewa nafasi ya ruhusa kuhamisha rasilimali hiyo ikiwemo Milango, Mabati na dhamani zingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Khamisi Nanswi alisema kuwa Halmashauri yake imepokea fedha kutoka Serikalini Tsh. Bilioni 8.07 kwaajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Soko kuu hilo.

"Tumepokea kutoka Serikali kuu Tsh. Bilioni 8.07 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi soko kuu la kisasa baada ya kukidhi vigezo licha ya kuwa Halmashauri zilizo wasilisha Serikalini maombi maalumu ya kuomba fedha zilikuwa nyinmgi kati yake Halmashauri 12 maombi yao yalikidhi vigezo nasisi tukiwemo", alisema Nyanswi.

Katika Mkoa wao wa Mara Halmashauri ya Tarime Mji ndiyo pekee ufanikiwa katika maombi hayo na Serikali kuridhia kuwapatia fedha hizo kwa hali hiyo wamewaomba Wafanyabiashara kuridhia na kupokea mradi pamoja na kuhama ili kupisha utekelezaji wa mradi ujenzi wa Soko la kisasa kuanza mara moja, mji huo utabadilika mandhari na wageni watapenda kwenda kututembelea.