Katibu mkuu wa Umoja wa Mataıfa azitaka nchi za Ulaya zıjıfunze kutoka Afrika

Antonio Guterres katibu mkuu wa Umoja wa mataifa amesema pamoja na changamoto zote zinazolikabili bara la Afrika, bara hilo limeacha milango yake wazi kwa wakimbizi. Katıbu huyo alizitaka nchi za Ulaya ambazo zimefunga milango yake kwa wakimbizi zijifunze kutoka kwa Afrika.

Guterres aliyasema hayo katika mkutano mkuu wa 32 wa viongozi wa nchi wanachama za Umoja wa Afrika, OAU. Mkutano huo ulifanyika mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Ajenda kuu ya mkutano wa OAU mwak huu nı " Wakimbizi na kinachowakimbiza kutoka maeneo yao".

Guterres alisema pıa kwamba Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa unakabiliwa na matatizo makuu 3 ambayo ni amani na usalama, maendeleo endelevu pmoja na mabadiliko ya hali ya hewa.