https://monetag.com/?ref_id=TTIb Katika historia ya nchi Lissu peke yake ndiye aliyetelekeza kesi - Waziri Lugola | Muungwana BLOG

Katika historia ya nchi Lissu peke yake ndiye aliyetelekeza kesi - Waziri Lugola


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kuwa kwa mara ya kwanza katika hostoria ya nchi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ndiye aliyetelekeza kesi yake.

Lugola amesema kuwa watu wenye kesi wamekuwa wakifuatilia sana kesi zao mpaka unawaonea huruma.

"Wenye kesi wamekuwa wakifuatilia sana kesi zao mpaka unawaonea huruma,lakini kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu Mh. Lissu ndiye peke yake ambaye ametelekeza kesi yake sasa unajiuliza wewe ndiye mwenye kesi alafu unaitelekeza," amesema Lugola katika mkuatano wake na waandishi wa habari jijini Arusha.

Aidha Lugola amehoji kuwa kwanini hataki kuja kwenye kesi yake Lissu, amedai kuwa hataki kuja kwasababu anajua nini nyuma ya pazia .

Lissu alishambuliwa mchana wa Septemba 7, 2017 akiwa ndani ya gari, nje ya makazi yake Area D, jijini Dodoma wakati akitoka kuhudhuria mkutano wa Bunge akiwa na dereva wake Adam Bakari ambaye hakujeruhiwa.