.

2/11/2019

Kesi ya Amber Rutty na Mumewe kuunguruma March 7


Kesi inayowakabili Msanii Rutyfiya Aboubakary maarufu Kama Amber Rutty na mume wake Said Mtopali ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile Upelelezi umekamilika na sasa kesi hiyo itaanza kuunguruma Machi 7 kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka ameeleza hayo leo Februari 11.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili Nguka amedai, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali. Kufuatia taarifa hiyo,  Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi March 7, 2019. Amber Rutty na mumewe walifikishwa mahakamani hapo November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.