.

2/14/2019

Kesi ya Mbowe, Matiko yasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema inasubiri uamuzi wa mahakama ya rufaa  kuhusu dhamana ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Kelvin Mhina ameeleza hayo wakati kesi hiyo ya kufanya mikusanyiko isiyo halali inayowakabili viongozi tisa wa CHADEMA, iliyokuja kwa ajili ya kutajwa.

viongozi wengine wa CHADEMA katika kesi hiyo ambao wapo nje kwa dhamana ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.